Tanzania Census 2022

"MTANDAO WA POSTA NI MTANDAO ULIOENEA DUNIA NZIMA HIVYO UMERAHISISHA UTUMAJI WA BIDHAA" Dkt. Jim Yonazi

"MTANDAO WA POSTA NI MTANDAO ULIOENEA DUNIA NZIMA HIVYO UMERAHISISHA UTUMAJI WA BIDHAA" -Dkt. Jim Yonazi 
 
 2 Jim
 
 
Leo Oktoba 08,2021.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amefungua semina kwa watoa huduma za mawasiliano, Semina hiyo imeandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ( UCSAF), Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta dunia yatakayo fanyika Oktoba 9.
 
Katika kuboresha upatikanaji wa huduma za Mawasiliano kwa Wananchi Mfuko wa Mawasiliano kwa wote umekuwa ukishirikiana  na Shirika la Posta kurahisisha upatikanaji wa huduma za Mawasiliano hasa kwa Wananchi waishio Vijijini. Mfuko wa Mawasiliano kwa wote unajukumu la kuhakikisha watoa huduma za vifurushi ambao wamesajiriwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  wanafika Vijijini pamoja na kufikisha huduma za TEHAMA kwa Wananchi.
 
Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa mtandao wa Posta ni mtandao ulienea dunia nzima hivyo umerahisisha utumaji wa bidhaa,
"Tukumbuke kwamba mtandao wa Posta ni mtandao ulioenea dunia nzima ndio maana utumaji wa bidhaa toka sehemu moja kwenye nyingine umefanikiwa kutokana na uwepo wa Posta." Dkt. Jim Yonazi 
 
"Kama ambavyo bidhaa zinatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo ndivyo Sekta ya Posta itaendelea kudumu katika maisha yetu na Serikali inaendelea kuunga mkono kuhakikisha Sekta ya Posta inaendelea kukua na kuleta mafanikio chanya ndani ya nchi." Alisema Dkt. Jim Yonazi 
 
"Tunaendelea kufanya mabadiliko katika Shirika la Posta kwa kuleta huduma ya Posta Kiganjani ili huduma za Posta zipatikane katika Simu yako ya Mkononi  na hapa ndipo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unapofanya kazi kuhakikisha hata yale maeneo yasio na huduma za Mawasiliano yanapata huduma hiyo ili kufanikisha dhana hii ya Huduma  Kiganjani Kwako." Alisema Dkt. Jim Yonazi 
 
Alimalizia kwa kuwaomba washiriki wote kuchukua maarifa kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kupeleka Maarifa hayo kwa wengine ili waweze kufahamu shughuli zinazofanywa na sekta hii pamoja na Sekta ya Mawasiliano kwa Ujumla.
 
 IMG 20211008 WA0113
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa semina hiyo. 
 
 
 IMG 20211008 WA0127
 
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) Bi. Justina Mashiba akizungumza wakati wa semina hiyo.
 
 
IMG 20211008 WA0102
 
Viongozi mbalimbali wa Shirika la Posta Tanzania wakiskiliza jambo wakati wa semina hiyo. 
 
 
IMG 20211008 WA0136
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akiwa kwenye picha ya Pamoja baada ya semina hiyo. 
 
 
 
PICHA ZAIDI ZA SEMINA HIYO: 
 
 IMG 20211008 WA0156
 
 
IMG 20211008 WA0163
 
 
IMG 20211008 WA0145
 
 
IMG 20211008 WA0160
 
 
IMG 20211008 WA0103
 
 
IMG 20211008 WA0162
 
 
IMG 20211008 WA0151
 
IMG 20211008 WA0154
 
 
IMG 20211008 WA0153
X

Tanzania Posts Corporation

You have no authorized to right click contents of TPC, All rights reserved!