📍POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA ATCL📍
POSTA YAFANYA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA NA ATCL
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Daniel Mbodo amekutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ndg. Ladislaus Matindi katika ofisi za ATCL, leo jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ambavyo taasisi hizi mbili zinavyoweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi hasa katika nyanja za usafirishaji wa mizigo, vifurushi na vipeto ndani na nje ya nchi pamoja na Ukataji wa tiketi za ndege kupitia mtandao wa posta ulioenea nchi nzima
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka Shirika la Posta Tanzania pamoja na Shirika la ndege Tanzania (ATCL)
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
08 Novemba, 2021.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Daniel Mbodo akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ndg. Ladislaus Matindi, mara baada ya kikao hicho, jijini Dar es Salaam