Loading . . .

News Single

News Single

NAIBU WAZIRI AFUNGUA JUKWAA LA TANO LA EACO LA POSTA NA LOGISTIKIA

Blog Single

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama, amefungua rasmi Jukwaa la Tano la EACO la Posta na Logistikia (EPLF 5), jijini Arusha, akisisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu katika kuboresha huduma za posta na kukuza biashara za kidijitali Afrika Mashariki.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Naibu Waziri amesema sekta ya posta na logistikia ina nafasi muhimu katika kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, biashara za mtandaoni na kuwaunganisha wafanyabiashara na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya malipo, ufuatiliaji wa mizigo na anwani za makazi, ikiwemo Mfumo wa Taifa wa Anwani za Makazi (NaPA), ili kuongeza ufanisi wa huduma na kurahisisha biashara zinazovuka mipaka.

Sambamba na hayo, Naibu Waziri, ametembelea mabanda ya maonesho na kuhimiza nchi wanachama wa EACO kushiriki zaidi katika maonesho yajayo kwa kuwasilisha ubunifu na teknolojia zinazoweza kuchochea uwekezaji na maendeleo ya sekta hiyo.

Shirika la Posta Tanzania (TPC) ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika maandalizi na utekelezaji wa jukwaa hilo, kwa kushirikiana na EACO, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na wadau wengine.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.