Loading . . .

News Single

News Single

BIASHARA YAKO INA SULUHISHO, EMS INAKUUNGANISHA NA WATEJA WAKO

Blog Single

Kutoka kwa wafanyabiashara hadi Taasisi mbalimbali, Shirika la Posta Tanzania linaendelea kuwafikia wateja wake jijini Dar es Salaam kupitia kampeni za moja kwa moja, zenye lengo la kuwafahamisha zaidi kuhusu fursa za usafirishaji zinazopatikana kupitia huduma bora ya EMS.

Katika kampeni hiyo, timu kutoka Shirika la Posta Tanzania, imekutana na wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali ikiwemo, Kinondoni, Tegeta, Mwenge, Makumbusho, Kunduchi, Magomeni, Kawe na Bunju kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu namna EMS inavyorahisisha usafirishaji wa bidhaa zao pamoja na nyaraka zote ndani na nje ya nchi.

Kwa wafanyabiashara wanaotaka kuwafikia wateja wao kwa urahisi zaidi na kupanua wigo wa masoko yao, EMS ni suluhisho lao katika kuwaunganisha na fursa za ndani ya nchi na za kimataifa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.