Loading . . .

News Single

News Single

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA KUTOKA UCSAF

Blog Single

Shirika la Posta Tanzania limepokea vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika hafla maalumu ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za kidijitali nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Switbert Zacharia Mkama, amesema vifaa hivyo vitakuwa nyenzo muhimu ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika maeneo yote nchini.

 

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na Sera ya Maendeleo ya Posta.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Bw. Mulembwa Denis Munaku, ameipongeza menejimenti ya Shirika la Posta kwa usimamizi mzuri wa huduma zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania.

Ameeleza kuwa, ununuzi na ukabidhi wa vifaa hivyo ni sehemu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na UCSAF ili kuwezesha vituo vya posta kufanya kazi kwa ufanisi na kuwapatia Watanzania huduma jumuishi za mawasiliano.

Naye Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Daniel Mbodo, ameushukuru mfuko wa UCSAF kwa kutoa vifaa hivyo huku akisisitiza kuwa vifaa hivyo vina umuhimu mkubwa katika kuimarisha huduma za posta na kuwasaidia wananchi kupata huduma jumuishi na salama zaidi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania