Loading . . .

News Single

News Single

FURSA ZA BIASHARA ZINAENDELEA KUFUNGUKA

Blog Single

Shirika la Posta Tanzania (TPC), kupitia Kitengo cha Masoko Mkoa wa Mbeya, limefanikisha ushirikiano wa kibiashara na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Mbeya, kupitia huduma ya EMS.

Ushirikiano huu unaweka msingi wa kuimarisha matumizi ya huduma za EMS katika shughuli za chuo, huku ukiwa sehemu ya mkakati wa TPC wa kupanua wigo wa wateja wa taasisi na kuongeza matumizi ya huduma zake za usafirishaji wa nyaraka na vifurushi.

Kupitia huduma ya EMS, TPC inalenga kuwawezesha wateja wa taasisi kupata suluhisho la kuaminika katika usafirishaji wa nyaraka na vifurushi, kwa kuzingatia mahitaji ya kasi, usalama na ufanisi wa huduma.

Ushirikiano na CBE Mbeya unaakisi juhudi za TPC za kujenga mahusiano ya kibiashara yenye thamani na taasisi za elimu, pamoja na kutambua fursa za kibiashara zinazotokana na mahitaji ya kila siku ya taasisi hizo.

TPC inaendelea kuhamasisha taasisi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutumia huduma zake kama sehemu ya kurahisisha shughuli zao za usafirishaji na mawasiliano ya kibiashara.

Katika picha: Mkurugenzi wa Kampasi ya CBE Mbeya, Dkt. Beny Mwenda (kushoto), akiwa pamoja na Abdon Mahimbo, Afisa Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (kulia), katika hatua za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kupitia huduma ya EMS.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.