JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

BODI YA WAKURUGENZI


...

BALOZI MEJA JENERALI MSTAAFU GAUDENCE SALIM MILANZI

MWENYEKITI WA BODI

Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Salim Milanzi, ni kiongozi mstaafu wa kijeshi mwenye zaidi ya miaka 40 ya utumishi katika uongozi wa kijeshi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akipita katika majukumu mbalimbali ikiwemo upangaji wa mikakati ya ulinzi wa Taifa, kulinda amani, na majukumu ya kidiplomasia. Mbali na Nyadhifa za Kijeshi amewahi kushika nyadhifa za juu serikalini ikiwemo ile ya Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Balozi Meja Jenerali Mstaafu Milanzi alianza taaluma yake katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 1977, ambapo alionyesha uongozi bora na kupanda vyeo hadi kufikia nafasi ya Meja Jenerali. Mara baada ya kustaafu kwake kutoka JWTZ, alifanikiwa kufanya kazi katika utumishi wa umma na kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Balozi Meja Jenerali Mstaafu Milanzi ana Shahada ya Uzamili katika Usalama na Masuala ya Kistratejia kutoka Chuo Kikuu cha Bangladesh cha Wataalamu (2012), Stashahada ya Uzamili ya Sheria inayozingatia Sheria za Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989), na Shahada ya Kwanza ya Mahusiano ya Kimataifa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988).

Michango yake katika kuzuia migogoro, kujenga amani, na ushirikiano wa kijeshi na kiraia inaheshimika sana na mashirika kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na taasisi za kikanda barani Afrika kama SADC.


Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA