JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


 

    USAFIRISHAJI WA KAWAIDA:

Kundi hili linahusisha usafirishaji ambao hupokea (Accept), husafirisha (Convey), na kusambaza (deliver) Barua, Vipeto, Mizigo na Vifurushi kwa njia ya kawaida kupitia njia ya maji na nchi kavu (meli, barabara na reli):

    1. Barua za Kawaida:

Hizi ni barua zisizozidi uzito wa kilogramu mbili (2kg), kwenda ndani na nje ya nchi. Barua hizi zinatakiwa kuwekwa Anwani ya mtumiwa kwa mbele na Anwani ya mtumaji kwa nyuma. Hata hivyo barua hizi haziwekwi alama/ namba ya ufuatiliaji (tracking number).

Barua za aina hii zinaweza kulipiwa kwa gharama nafuu (economy mail) au gharama za kupewa kipaumbele (priority mail)

    1. Rejesta:

Hizi rejesta hazizidi uzito wa kilogramu mbili (2kgs). Ili iitwe rejesta lazima iwekwe namba maalum ya ufuatiliaji (tracking number) yenye kuanza na neno RD na kuishia na neno TZ kwa rejesta za ndani au RR na kuishia na neno TZ kwa rejesta za kimataifa. Barua za aina hii huashiria kuwekwa vitu vya thamani ndani yake kama hati, vyeti, nk.

    1. Vipeto:

Vipeto vina tofauti na barua za kawaida kwa kuwa huwa na vitu vya thamani ndani mwake na kufungwa kama kifurushi kidogo chini ya kilo tatu (3Kgs). Huwekwa namba maalum ya ufuatiliaji (tracking number) kwa mtiririko wa vipeto.

    1. Vifurushi vya kawaida:

Vifurushi vya kawaida huanzia uzito unaozidi kilo 3 hadi kilo 30. Huwekwa namba maalum ya ufuatiliaji (tracking number) kwa vifurushi vya nchini na vya

kimataifa. Vifurushi vya kimataifa lazima vifungwe mbele ya afisa wa Posta na maafisa Ushuru wa Forodha ili kuorodhesha kwa uhakika vitu vilivyofungwa ndani ya kifurushi. Kufanya hivi husaidia kujaza fomu ya kiapo (declaration form) inayoambatana na kifurushi husika ili kifurushi kitakapofika nchi kinapokwenda mteja aweze kukadiriwa ushuru wa forodha kwa urahisi.

 

 

    1.  Mifuko ya Barua (M- Bag):

Huduma hii ni ya kusafirisha mizigo kwenye mfuko maalum kwa lengo la kurejesha au kutanguliza mizigo ya mtu aliyekwenda kwa shughuli maalum nje ya nchi yake.

    1. Posta Mlangoni:

Barua za posta mlangoni hupelekwa kwa kawaida na barua kufikishwa hadi nyumbani kulingana na Anwani za Makazi. Hivyo barua, nyaraka na vifurushi vya wateja kutoka ndani na nje ya nchi na husafirishwa na kufikishwa hadi nyumbani au ofisini kwa gharama nafuu kwa kutumia Anwani za Makazi na Postikodi.

  1.                 g. Mizigo ya Posta (Post Cargo):

Ni huduma maalum kwa ajili ya usafirishaji mizigo yenye uzito mkubwa zaidi ya kilogram 30 au yenye umbo lisiloweza kufungwa kama kifurushi na kutumwa Posta. Huduma hii ni nzuri kwa wateja wenye mizigo ya aina hii na wanaohamisha mizigo mikubwa kama samani za ndani, nafaka, biashara, nk

  1.                  h. Nyaraka au maandishi kwa wasioona:

Shirika hutoa huduma maalum kwa wateja wanaotuma au kutumiwa nyaraka au maandishi kwa wasioona (literature for the blind). Huduma hii ni bure. Hii ni kutokana na mkataba maalumu wa Umoja wa Posta Duniani kuwa nyaraka hizi zisafirishwe bure na Posta zote teule(designated postal Operators) za Serikali.

 

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA