JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


 

VITUO VYA HUDUMA PAMOJA

Serikali ina lengo la kuboresha utoaji wa huduma zake kwa kuwapunguzia wananchi muda mrefu na gharama za kutafuta huduma hizo. Hivyo Serikali imeanzisha Vituo vya Huduma Pamoja vinavyowezesha upatikanaji wa huduma za Serikali katika eneo moja ndani ya majengo ya Ofisi za Shirika la Posta Tanzania. Lengo kuu ni kufanya maboresho na mageuzi katika utoaji huduma kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano baina ya Taasisi za Serikali.

Huduma zitolewazo kwenye vituo vya Huduma Pamoja kwa sasa ni:-

  • Vyeti vya kuzaliwa na kifo - RITA;
  • Utoaji wa Pasipoti-UHAMIAJI;
  • Utoaji wa Kitambulisho cha Taifa-NIDA;
  • Usajili     wa kampuni za Biashara-BRELA;
  • Utoaji wa  Namba ya Mlipa Kodi (TIN)-TRA;
  • Taarifa za pensheni ya uzeeni, kujisali, uhakiki taarifa-PSSSF&NSSF; na
  • Utoaji wa Taarifa ya mali iliyopote na uhakiki kwa ajili ya kupata leseni za udereva – Jeshi la Polisi Tanzania TPF.
  • Utoaji wa Leseni za Biashara za Halmashauri ya Jiji Dodoma

 

 

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA