JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


 

BIASHARA MTANDAO

Biashara mtandao ni huduma za kidijitali zinazotolewa na Shirika kwa ajili ya kukuza na kuimarisha biashara za wajasiriamali na makampuni yanayotaka kufanya biashara mtandao. Biashara mtandao ipo kwenye Duka Mtandao la Posta, Uuzaji wa Stempu mtandaoni na Uuzaji wa Stempu za maonesho (philatelic stamps) mtandaoni.

Upatikanaji wake ni wa kidijitali kupitia njia zifuatazo:

    1. Duka mtandao kupitia www.postashoptz.post

Ni huduma ya kuuza, kununua na kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwa njia ya mtandao wa pamoja ulioanzishwa na Shirika la Posta Tanzania na duka hili limeunganishwa na linapatikana kwenye nchi 192 duniani zilizopo chini ya umoja wa Posta duniani (UPU). Duka hili linatumia lugha zaidi ya 20 ambazo hutumika kuwasiliana na mataifa mbalimbali. Mfanyabiashara/mjasiriamali anaweza kujisajili kupitia tovuti www.postashoptz.post. Duka hili limekuwa msaada mkubwa sana kwa wajasiriamali katika kukuza biashara zao kwa kuwafikia wateja wengi duniani.

    1. Uuzaji wa Stempu mtandaoni

Uuzaji wa stempu hufanyika posta au mtandaoni ambapo hupatikana kwenye duka mtandao www.stemps.tz.post. na mnunuzi kupelekewa mahali alipo. Stempu ni bidhaa ambayo huwakilisha mambo matatu: Bidhaa, Gharama za Usafirishaji na Balozi wa Nchi. Huonesha utalii wa nchi, uchumi wa nchi, shughuli za kijamii, historia, vipaji (talents) vya wananchi, nk.

Aidha, Stempu huonesha maeneo ya urithi, wanyama, mimea, mbuga za wanyama, watu maarufu n.k. ambayo hulipwa fedha sawa na kiasi kinacholingana na thamani yake kabla haijatumiwa katika barua au nyaraka.

    1. Uuzaji wa Stempu za wakusanyaji/maonesho mtandaoni (e-philatelic stamps)

Ni huduma ya kuuza stempu za mtandaoni kupitia duka linalopatikana kupitia tovuti www.stamps.tz.post. Wanunuzi/ wakusanyaji (stamp collectors) wanaweza kuonesha au kuuza stempu kwa wateja wengine.

Ukusanyaji wa stempu ni sehemu ya utafiti wa stempu za posta, alama za posta na nyenzo zinazohusiana na hizo. Ukusanyaji wa stempu ni shauku ya kielimu sana, inahusisha mkusanyiko wa stempu na utunzaji wa stempu za miaka mbalimbali kwa mpangilio mzuri.

Ukusanyaji wa stempu umekuwepo kwa miaka mingi, ilikuwa ni lazima mtu atumie pesa kununua, kubadilishana au kupata stempu za matoleo mbalimbali. Leo wakusanyaji wanaweza kuuza stempu hizo kwa bei ya juu sana kwenye soko la philatelic stamps. Ukusanyaji wa stempu bado hubaki kuwa ni tabia ya kurithisha kwa mkusanya stempu mwenyewe.

  1.                  d.  Huduma ya vituo vya Intaneti (Internet Café)

Ni huduma inayotolewa kwa wateja wanao hitaji huduma za mtandao kupitia intaneti zilizo katika ofisi za Posta. Huduma zitolewazo ni kudurufu nyaraka na zingine kama kuchapisha, kusambaza na kuvinjari mtandaoni (Printing, Scanning, Surfing/ Browsing).

  1.  Sanduku la kielekitronic (Virtual Box)

Ni huduma ya kumiliki sanduku la kielekitronic kwa njia ya mtandao, ambapo mteja atasajili namba yake ya simu kuwa sanduku la Posta kwa kutumia simu ya mkononi, kishkwambi au kompyuta mpakato (Laptop). Huduma hii inapatikana kupitia mfumo wa Posta Kiganjani.

 

Mteja anaweza kujisajili kama:

  • Mtu binafsi (Individua customer). Kujisajili ni Tsh.14,160/=

  • Kampuni (Corporate customer).  Kusajili gharama yake ni    Tsh.59,000/=

Mteja atajisajili kupitia “Appstore”, “Playstore”, Postawebsite: www.posta.co.tz au link: https://postakiganjani.posta.co.tz.

 

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA