JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Maswali yanayoulizwa mara nyingi...

Shirika la Posta Tanzania, limeteuliwa kama mtoa huduma za Posta na usafirishaji Nchini;

Huduma zinazotolewa na Shirika ni Pamoja na:

  1. Huduma za Usafirishaji wa Kawaida
  2. Huduma za Usafirishaji wa Haraka
  3. Huduma za Uwakala na Fedha
  4. Duka la Kubadilishia fedha za Kigeni
  5. Biashara Mtandao
  6. Upangishaji wa Miliki
  7. Uwekezaji
  8. Huduma Pamoja

 

Ndiyo, EMS ni huduma ya barua na usafirishaji ya kasi ya juu inayopatikana ndani na Nje ya Nchi. EMS ni miongoni mwa huduma za Shirika la Posta zenye bei ya juu ikilinganishwa na huduma zingine za barua na usafirishaji kutokana na aina ya usafirishaji wake (Express).

Ili kupata gharama za kutuma barua na vifurushi ndani na nje ya nchi, tafadhali bonyeza linki hii kupata huduma zetu;

https://posta.co.tz/index.php/tariffs

 

Tafadhali bofya tovuti hii na fuata maelekezo ya namna ya kujiunga,

Jaza taarifa zinazohitajika na ufuate maelekezo.

https://smartposta.posta.co.tz/ ( https://smartposta.posta.co.tz/ )

 

Wasiliana na ofisi za Posta Nchi nzima kupitia linki afuatayo:

https://posta.co.tz/index.php/contact-us (https://posta.co.tz/index.php/contact-us)

 

 

 

 

Hili ni jukwaa la biashara mtandao linamuwezesha mteja kuingia na kuchagua bidhaa anayotaka kisha kuinunua kwa njia ya kielektroniki na kuchagua njia ya usafirishaji wa Posta ndani ya duka hili, ambapo kupitia usafirishaji huo, mteja atapelekewa bidhaa zake hadi mahali alipotaka bidhaa yake ifike. Aidha jukwaa hili lenye usalama mkubwa wa biashara mtandao linawawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati kuweka na kutangaza bidhaa zao ndani ya jukwaa hili bure.

 

Ndugu mteja bonyeza linki ifuatayo kupata maelezo zaidi ya duka la posta mtandao.

 

 https://www.postashoptz.post/

 

Ndiyo, na ni rahisi kwa mtu anaweza kuomba sanduku kupitia tovuti yetu bofya linki ifuatayo, kisha jaza taarifa zianazohitajika kwa usahihi.

 https://smartposta.posta.co.tz/( https://smartposta.posta.co.tz/ ) 

Ndio, unaweza kupata huduma za Leseni ya udereva kupitia dirisha la TRA lililoko ndani ya Ofisi za Posta. Kwasasa vituo ni viwili tu, Dar es Salaam na Dodoma.

Aidha Shirika kupitia Vituo vya Huduma Pamoja vinatoa huduma nyingine kama vile;

  • Utoaji wa  Namba ya Mlipa Kodi (TIN)-TRA;
  • Vyeti vya kuzaliwa na kifo - RITA;
  • Utoaji wa Pasipoti-UHAMIAJI;
  • Utoaji wa Kitambulisho cha Taifa-NIDA;
  • Usajili     wa kampuni za Biashara-BRELA;
  • Taarifa za pensheni ya uzeeni, kujisali, uhakiki taarifa-PSSSF&NSSF; na
  • Utoaji wa Taarifa ya mali iliyopote na uhakiki kwa ajili ya kupata leseni za udereva – Jeshi la Polisi Tanzania TPF.
  • Utoaji wa Leseni za Biashara za Halmashauri ya Jiji Dodoma

Serikali imeanzisha Vituo vya Huduma Pamoja vinavyowezesha upatikanaji wa huduma za Serikali katika eneo moja ndani ya majengo ya Ofisi za Shirika la Posta Tanzania.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA