JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA


 

      USAFIRISHAJI WA HARAKA

Kundi hili linahusisha usafirishaji ambao hupokea (Accept), husafirisha(Convey), na kusambaza(deliver) Nyaraka, Vipeto na Vifurushi kwa njia ya haraka ambao hufanywa kwa ndege au usafiri wa haraka uliopo  kutegemea na maeneo. Usafirishaji huu hufanyika kwenye huduma zifuatazo:

    1. Nyaraka za EMS:

Ni huduma ya kusafirisha na kusambaza nyaraka na vipeto muhimu kwa haraka na usalama ndani na nje ya nchi kwa malipo yanayowezesha kufikishwa hadi nyumbani. Kila nyaraka ya EMS huwekwa namba maalum ya ufuatiliaji (tracking number) yenye kuanza na neno EE na kuishia na neno TZ kwa huduma hii mpokeaji hutakiwa kusaini ili kuthibitisha amepokea nyaraka husika.

 

 

    1. Vifurushi vya EMS:

Ni huduma ya kusafirisha na kusambaza vifurushi kwa haraka na usalama ndani na nje ya nchi kwa malipo yanayowezesha kufikishwa hadi nyumbani. Kila kifurushi cha EMS huwekwa namba maalum ya ufuatiliaji (tracking number) yenye kuanza na EE na kuishia na neno TZ kwa huduma hii Mpokeaji hutakiwa kusaini kuthibitisha kuwa kifushi chake kimepokelewa.

    1. Barua za Haraka kwenye Miji (Posta City Urgent Mail-pCUM):

Ni huduma ya kusafirisha barua, virufushi na nyaraka ndani ya miji au jiji kutoka kwa mteja na kupelekwa moja kwa moja kwa mteja anayetakiwa kupokea pasipo kupitisha kuchakatwa kwenye ofisi za Posta.

    1. Usambazaji wa Sampuli za Maabara:

Shirika la Posta limepewa jukumu na Wizara ya Afya ili kupokea, kusafirisha na kufikisha sampuli za maabara kutoka kwenye vituo vidogo na kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo na kurudisha majibu kwa haraka. Huduma hii husaidia wananchi kupata majibu ya vipimo kwa wakati.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA