Habari
MAADHIMISHO YA MIAKA 20
Shirika la Posta Tanzania limeanza kushiriki rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Katika siku ya kwanza ya maadhimisho hayo, Posta Tanzania pamoja na taasisi mbalimbali zilizopata mwaliko walitembelea ghala teule la mfumo wa stakabadhi za ghala lililopo Nala, Dodoma, kwa ajili ya ziara ya mafunzo na kujifunza namna mfumo huo unavyorahisisha biashara, uhifadhi wa mazao pamoja na upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wadau mbalimbali.
Ziara hiyo imekuwa sehemu ya ratiba ya ufunguzi wa maadhimisho hayo yanayolenga kuonyesha mafanikio ya mfumo wa stakabadhi za ghala katika kukuza uchumi na biashara nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

