JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TUMESOGEZA HUDUMA KARIBU ZAIDI


Katika juhudi za kuboresha upatikanaji wa huduma za umma, Shirika la Posta Tanzania linaendelea kutekeleza mpango wa Huduma Pamoja unaowawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za Serikali katika eneo moja.

Kupitia vituo vya Huduma Pamoja vilivyopo katika ofisi za Posta nchini, wananchi wanapata huduma kwa urahisi bila kulazimika kutembelea ofisi nyingi au kusafiri umbali mrefu. Mpango huu umechangia kupunguza muda na gharama, huku ukiboresha uzoefu wa wananchi katika kupata huduma za Serikali.

Kwa kutumia mtandao mpana wa ofisi za Posta, Huduma Pamoja inaendelea kusogeza huduma karibu na wananchi na kuunga mkono agenda ya Serikali ya kutumia teknolojia, ubunifu na miundombinu iliyopo kuboresha utoaji wa huduma za umma.

Huduma Pamoja: huduma za Serikali karibu na wananchi.

Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA