Habari
UHUSIANO NA WATEJA WAIMARIKA
Timu ya Masoko na Mauzo ya Shirika la Posta Tanzania imeendelea kuimarisha uhusiano na wateja wakubwa kwa kufanya kikao na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dodoma, katika juhudi za kutangaza huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na Shirika.
Timu ya hiyo imepata fursa ya kukutana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuimarisha matumizi ya huduma za Posta katika shughuli za taasisi hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Mauzo wa Shirika la Posta, Bw. Philip Kowero, amemueleza Bw. Kijazi, kuhusu maboresho na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Shirika la Posta katika huduma zake, hususani huduma ya EMS.
Kwa upande wake Bw. Kijazi ameonyeshaa kuridhishwa na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Shirika la Posta, akitaja huduma ya EMS kama huduma ambayo imeendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya wateja katika mazingira ya sasa.
Ameeleza kuwa mabadiliko yanayoonekana katika huduma za Posta ni hatua muhimu katika kuhakikisha Shirika linaendana na mahitaji ya sasa ya wateja pamoja na kasi ya maendeleo ya teknolojia.
Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

