JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

WARSHA YA UPU YA KUJIKINGA NA MAAFA


Katika siku ya pili ya warsha ya mpango wa kukabiliana na majanga, Bw. David Andrea (Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti wa Vihatarishi na Ubora) akiwakilisha Shirika la Posta Tanzania (TPC), aliwasilisha maelezo ya kina jinsi TPC inavyojiandaa na kukabiliana na majanga.

Bw. David Andrea alieleza uzoefu wa Tanzania katika kukumbwa na mafuriko mara kwa mara, akielezea tukio la mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokea Hanang mwezi Desemba 2023, ambayo yalisabaisha vifo na uharibifu wa miundombinu, hususani Ofisi ya Posta Hanang. Tukio hili lilionyesha haja ya haraka ya kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na majanga.

Bw. Andrea alieleza jinsi TPC ilivyojikita katika kuimarisha miundombinu, kuwaongezea ujuzi wafanyakazi na kutekeleza Mpango wa Kuendelea kwa Shughuli za Kibiashara (BCP) ili kuhakikisha shughuli zinaweza kuendelea haraka baada ya maafa.

Katika hitimisho lake, Bw. Andrea alishukuru mchango wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) katika kuboresha uimara wa TPC kupitia mafunzo ya kujenga uwezo na ushirikiano wa kiteknolojia. Pia alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa timu, maandalizi na uimara katika mtandao wa posta.
 
 
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA