JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

MAFUNZO YA NDHAMU YATOLEWA


Wawakilishi wa watumishi wa Shirika la Posta Tanzania kutoka Kanda, chini ya Chama cha Wafanyakazi, COTWU (T), wamepewa mafunzo kuhusu nidhamu kazini ambayo yamefanyika katika Hoteli ya PH Executive, mjini Morogoro, Leo Mei, 21 2026.

Mafunzo hayo yametolewa na Bw. Kindamba kutoka Ofisi ya Kurugenzi ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kuhusiana na masuala ya Nidhamu mahali pa kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma.

Washiriki wamejifunza kuhusu Mamlaka ya nidhamu katika Utumishi wa Umma, Hatua za kinidhamu kwa Makosa makubwa na madogo pamoja na adhabu zake. 

Aidha, mafunzo hayo yametumia mbinu shirikishi ikiwemo majadiliano, mifano halisi, maswali na majibu ili kuongeza uelewa wa vitendo.

Washiriki wameahidi kutumia maarifa hayo kwa kwenda na kuwaelimisha watumishi kutoka katika Kanda zao na kuwapa mrejesho kuhusiana na masuala haya ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma. 

Imetolewa na;
Idara ya Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA