JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

EMS NDANI YA MWISHO WA RELI NA KIBIRIZ


Timu ya Masoko na Mauzo imendelea kutoa elimu kuhusu huduma ya Usafirishaji wa Vifurushi kwa njia ya haraka (EMS) kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma, kupitia Kampeni ya mtaa Kwa mtaa katika maeneo ya Stesheni ya Kigoma na Kibirizi.

Katika zoezi hilo, wafanyabiashara wamepewa elimu kuhusu namna wanavyoweza kutumia huduma ya EMS kusafirisha bidhaa mbalimbali za biashara kwa usalama na ufanisi kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Miongoni mwa bidhaa zinazoweza kusafirishwa kupitia EMS ni dagaa, samaki na bidhaa nyingine za biashara, ambazo wafanyabiashara wa Kigoma wanaweza kuzifikisha katika masoko ya kimataifa, ikiwemo Marekani, Canada, Ubelegiji pamoja na maeneo mengine duniani.

Huduma hiyo inalenga kuwawezesha wafanyabiashara wa Kigoma kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika Mkoa huo, hususani kutokana na shughuli za uvuvi na biashara zinazofanyika katika ukanda wa Ziwa Tanganyika, kwa kuwaunganisha na masoko ya ndani na kimataifa.

Shirika la Posta Tanzania linaendelea kuhamasisha wafanyabiashara kutumia EMS kama njia ya kupeleka bidhaa zao kwa haraka, usalama na uhakika, hatua inayoweza kuchangia kukuza biashara zao na kuongeza wigo wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa Kigoma.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA