JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

AMSHA AMSHA ZA KITAA SABASABA 2026


Leo tumefikia hitimisho la kampeni ya Amsha Amsha za Kitaa iliyodumu kwa wiki tatu kuelekea Maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara SABASABA 2026.

Kupitia kampeni hii, Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na TANTRADE limeendelea kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu huduma zitakazorahisisha ushiriki wa wadau na wananchi katika kipindi chote cha maonesho ya SABASABA.

Shirika la Posta Tanzania litaendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma za PostCargo kwa usafirishaji wa mizigo mikubwa, Royal Buggies kwa huduma za usafiri ndani ya viwanja vya maonesho, pamoja na Swifpack kwa huduma za usafiri wa kuRequest kwa njia ya mtandao.

Tunakushukuru kwa kuwa sehemu ya safari hii ya uhamasishaji. Tukutane Sabasaba 2026 tukifurahia huduma bora, za kisasa na zenye uhakika kutoka Shirika la Posta Tanzania.

Imetolewa na;

Kitengo Cha Mawasiliano,

Shirika ala Posta Tanzania.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA