Habari
UKAGUZI WA SHUGHULI ZA SABASABA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Salim Milanzi, ameendelea na ziara yake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) kwa kukagua shughuli mbalimbali zinazotolewa na Shirika ndani ya viwanja vya maonesho, mara baada ya kukagua banda la Shirika.

Akiambatana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Macrice Mbodo, Mwenyekiti alijionea utoaji wa huduma za usafirishaji kupitia PostCargo, SwiftPack, scooters na Bajaji ndani ya viwanja vya Sabasaba.

Baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti, amepongeza ubora wa huduma hizo na kuwahimiza watumishi kuendelea kutoa huduma kwa weledi, ufanisi na kuendelea kuitangaza Posta Tanzania kupitia Maonesho ya Sabasaba.

Imeandaliwa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania

