JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC YAPOKEA UGENI WA BALOZI WA ITALIA


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo amepokea ugeni wa Balozi ya Italia nchini Tanzania  Bw. Giuseppe Sean Coppola leo tarehe 13 May 2025.

Mhe.Balozi Coppola ametembelea Shirika akiambatana na Naibu Balozi, Bw. Davide Lorenzini pamoja na Afisa Utawala Ubalozi wa Italy Bi. Caterina Comisini.

Ugeni huo ulifanya mazungumzo na Bw. Mbodo ofisini kwake ambapo wamejadili ushirikiano wa kibiashara ambao Shirika litatoa huduma za posta kwa ubalozi wa Italia nchini ikiwemo huduma za usafirishaji wa Mabalo ya Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Italia unaotarajiwa hivi karibuni.

Katika mazungumzo Hayo Postamasta Mkuu aliambatana na Bw. Elia Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta kimataifa , Bw. Ahmad Rashid, Meneja wa EMS na Bw. Ferdinand Kabyamela, Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA