Habari
KIREDIO ATEMBELEA BANDA LA POSTA
Mtengeneza maudhui, Kiredio, ametembelea banda la Shirika la Posta Tanzania katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo alipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo pamoja na maboresho ya kidijitali yanayolenga kurahisisha huduma kwa wananchi.

Akiwa katika banda la Posta, Kiredio alipata fursa ya kufahamishwa kuhusu huduma za posta, usafirishaji wa vifurushi na mizigo, huduma za kidijitali pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania.

Banda la Shirika la Posta Tanzania linaendelea kuvutia wageni mbalimbali, wakiwemo viongozi, wafanyabiashara, wadau na watengeneza maudhui, wanaofika kujionea ubunifu na huduma zinazotolewa na Shirika hilo katika Maonesho ya Sabasaba mwaka 2026.

Imeandaliwa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

