Habari
NGUMI MPYA YA MANDONGA IMEFIKA
Mcheza ngumi maarufu nchini, Bw. Karim Mandonga, ametembelea banda la Shirika la Posta Tanzania katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), ambapo alipokelewa na Meneja wa Banda hilo ambaye pia ni Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Mshanga.

Wakati wa ziara hiyo, Mandonga alipatiwa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la Posta, ikiwemo huduma zinazopatikana ndani ya viwanja vya maonesho pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na shirika nchini kote.

Ziara hiyo imeendelea kuongeza mvuto wa banda la Posta, huku ikiwapa wageni fursa ya kujifunza zaidi kuhusu huduma za kisasa zinazotolewa na shirika kwa wananchi na wadau mbalimbali.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

