JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

WAZIRI SILAA ATEMBELEA BANDA LA POSTA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa akiambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya) Mhe. Dkt. Festo John Dugange wametembelea Banda la Posta katika Maonesho ya Wiki ya Anwani za Makazi yanayoendelea katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. 

Wakipokea maelezo ya kutoka kwa Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo ameeleza namna Mfumo wa Anwani za Makazi umekuwa msaada kwa Shirika la Posta Tanzania kwani mteja kupitia huduma mpya ya Posta ijulikanayo kwa jina la Swifpack anaweza kufikishiwa mzigo wake hadi mahali alipo.

Aidha, Bw. Mbodo ameelezea huduma mpya ya Posta ijulikanayo kwa jina la Swifpack inavyomwezesha mteja ambavyo inakatika banda la Posta wakati wa maonesho ya Wiki ya Anwani za Makazi leo tarehe 06 Februari jijini Dodoma.

Shirika la Posta Tanzania linashiriki Maonesho ya Wiki ya Anwani za Makazi yaliyozinduliwa Rasmi na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa (Mb) leo Februari 6, 2025 yatakayofanyika kwa siku tatu hadi Februari 8, 2025 katika Viwanja hivyo vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA