JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

Bw. ANDULILE ATEMBELEA OFISI ZA POSTA


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika Bw. Andulile Mwakalyelye ametembelea Ofisi za Posta Mkoa wa Dar es salaam ili kujione utendaji wa Shirika.

Akiwa katika ziara yake mkoani Dar es salaam amepokelewa na Meneja wa Posta wa mkoa huo Bw. Athumani Msilikale leo tarehe 3 Oktoba, 2023. Jijini Dar es salaam.

Bw. Mwakalyelye aliweza kujionea shughuli mbalimbali za utendaji ikiwemo Ofisi inayohusika na Mizigo ya Kimataifa (Dar es salaam Office of Exchange) na pia aliweza kuona ni  namna gani usafirishaji wa Virufushi na vipeto ndani na nje ya nchi unafanyika kwa kupitia Shirika la Posta Tanzania. 

Mjumbe huyo wa Bodi ya Shirika  aliambatana na Mratibu wa Shughuli za Mikoa ( Field Coordinator) Bw. Khamis Swedi kutoka Makao Makuu pamoja na Meneja Barua Mkoa wa Dar es salaam Bw. Julius Chifungo.

Katika ziara hiyo Bw. Mwakalyelye pia alitembelea Ofisi ya Mzizima ambapo alipokelewa na Meneja wa ofisi hiyo Bi. Rehema Mbunda na kupata nafasi ya kuongea na watendaji  wa ofisi hiyo na kujifunza jinsi wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku. Bwana Mwakalyelye alipata nafasi ya kuwasikiliza watumishi wa ofisi hiyo ili Kujua changamoto wanazokutana  nazo wakati wa  utoaji wa huduma kwa wateja wetu.

Pia  Bw. Andulile anatarajia kuendelea na ziara yake Ofisi za Posta Mikoa wa  Lindi na Mtwara ambapo atajionea utekelezaji wa majukumu yao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Masoko na Mahusiano
Shirika La Posta Tanzania
03 Oktoba, 2023.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA