JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

MSIMU WA SIKUKUU WAZIDI KUPAMBA MOTO


Katika msimu huu wa sikukuu, Shirika la Posta Tanzania limeeleza rasmi kuwa kuanzia sasa jezi halali za Klabu ya Simba SC kupitia ofisi zake nchi nzima zitauzwa kwa bei maalum ya shilingi 12,000 tu

Akizungumza leo tarehe 16 Desemba 2025 katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Ferdinand Kabyemelea ametoa wito kwa wananchi wote, hususan mashabiki wa Simba, kujitokeza mapema kununua jezi hizo kupitia ofisi za Posta.

                   

Kwa upande wa Simba SC, Msemaji wa Klabu hiyo Bw. Ahmed Ally amesema wameona kuna umuhimu wa kushirikiana na Posta ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, kwa kuwa Posta ni taasisi yenye mtandao mpana nchi nzima na inayoaminika.  

Ofa hii maalum ya msimu wa sikukuu imeanza leo tarehe 16 Disemba 2025 hadi tarehe 30 Januari 2026.

Imetolewa na:  
Kitengo cha Mawasiliano,  
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA