Habari
MWENYEKITI ATEMBELEA BANDA LA POSTA
Balozi Meja Jenerali (Mstaafu) Gaudence Salim Milanzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), atembelea banda la Shirika hilo tarehe 10 Aprili 2026 katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 ya mawasiliano iliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma. Katika ziara hiyo, Mwenyekiti alipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika, ikiwemo huduma za kidijitali na usafirishaji wa vifurushi kupitia mfumo wa SwifPack. Aidha, alipatiwa maelezo kuhusu namna huduma hizo zinavyochangia kurahisisha mawasiliano na usafirishaji nchini, sambamba na kuendana na maendeleo ya teknolojia ya kidijitali. Ziara hiyo inaonesha dhamira ya uongozi wa Shirika katika kufuatilia na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Posta Tanzania

