Habari
ONGEZENI TIJA NA UWAJIBIKAJI–RUVUMBAGU

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Toyi Aloyce Ruvumbagu, amewataka viongozi wa Shirika la Posta kuongeza tija, ubunifu na uwajibikaji ili kufanikisha malengo ya Shirika na kutoa huduma bora kwa taifa.
Amezungumza hayo leo tarehe 21 Julai 2025 wakati wa ufunguzi wa kikao cha 6 cha Extended Management kilichowakutanisha Wakuu wa Idara, Vitengo, Mameneja wa Mikoa yote na Meneja Mkaazi Zanzibar, katika Makao Makuu ya Shirika la Posta, jijini Dar es Sal jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake ya ufunguzi aliyomwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika Bw. Ruvumbagu alisisitiza umuhimu wa viongozi kujitathmini na kutekeleza majukumu yao kwa weledi. Amewataka Viongozi hao kuimarisha utendaji, kuzingatia maadili ya uongozi, na kuweka juhudi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha Shirika linatoa huduma stahiki na kuleta tija kwa umma na taifa kwa ujumla.
Makamu Mwenyekiti alihimiza viongozi kutathmini ufanisi wao na kujitathmini binafsi kuhusu nafasi zao, akisisitiza kuwa Shirika linatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kimkakati, kiutendaji na kimaslahi, hivyo wanapaswa kuongeza ubunifu na uwajibikaji katika nafasi zao.
“Serikali ina matarajio makubwa kwetu. Tusiwape nafasi wengine kutufanyia tunayoweza kuyatimiza sisi wenyewe!” – alisisistiza Bw. Ruvumbagu
Katika hatua nyingine Bw. Ruvumbagu ametumia nafasi hiyo kupongeza Shirika kwa kazi nzuri iliyoanza kuonekana na kusisitiza kuwa Bodi ya wakurugenzi imefurahishwa na mageuzi yanayoendelea kufanyika huku akisema kuwa inaleta matumaini ya kufika tunapotaka kwenda.
Kwa upande wake Postamasta Mkuu, Bw. Macrice D. Mbodo, amesisitiza umuhimu wa viongozi wote wa Shirika kufanya tathmini ya utendaji kwa mwaka 2024/2025, kujifunza kutoka katika changamoto na kuimarisha uwajibikaji katika mwaka mpya wa fedha 2025/2026.
Kikao hiki kinalenga kujadili taarifa ya utendaji wa biashara, tathmini ya mkataba wa utendaji kati ya Postamasta Mkuu na Bodi ya Wakurugenzi, na utambuzi wa watumishi hodari kitaifa.
Bw. Toyi Ruvumbavu(kulia), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika, wakati wa kikao cha wakati wa kufungua kikao cha 6 cha kawaida cha extended management, Tarehe 21 Julai 2025, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Macrice Mbodo (kushoto)Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, akizungumza wakati wa kikao cha wakati wa kufungua kikao cha 6 cha kawaida cha extended management, Tarehe 21 Julai 2025, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Toyi Ruvumbavu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania