JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA WAASWA KUWAJIBIKA KIUTENDAJI


Dodoma

POSTA WAASWA KUWAJIBIKA KIUTENDAJI

Msajili wa Hazina Ndg. Mgonya Benedicto awataka wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania kuwajibika ipasavyo katika utendaji wao ili kuhakikisha Shirika linatoa huduma stahiki kulingana na mahitaji ya sasa ya wananchi.

Ametoa agizo hilo tarehe 15 Januari, 2023, wakati akifunga Mkutano wa  29 wa Baraza Kuu la wa Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Markdon, jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo Ndg. Benedicto amesisitiza wafanyakazi hao kuwa na bidii na weledi katika utendaji wao ili kuendeleza juhudi za Serikali pamoja na Viongozi wa Shirika la Posta katika kuweka mazingira wezeshi kwa Shirika hilo yenye kulenga kukidhi mahitaji ya Posta katika mazingira ya sasa ya Teknolojia duniani.

Aidha, Ndg. Benedicto ameongeza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya msajili wa Hazina itaendelea kuunga mkono jitihada za Shirika la Posta nchini katika utatuzi wa changamoto na kuendelea kuliwezesha Shirika kuwa la kisasa na la Kidijitali ili liweze kuhudumia wananchi  sambamba na mahitaji yao.

Kwa upande wake Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Macrice Mbodo ameishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa jitihada mbalimbali inazozifanya katika kuliwezesha Shirika kupata mtaji na kusafisha mizania yake ili kukidhi matakwa ya uanzishwaji wake ya kuwahudumia wananchi na kutoa gawio kwa Serikali.


*Imetolewa na:*
*Kitengo cha Mawasiliano,*
*Shirika la Posta Tanzania*
*15 Januari, 2023*

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA