JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA YAINGIA MAKUBALIANO NA ZBC


SHIRIKA LA POSTA LAINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA ZBC

Shirikia la Posta Tanzania limeingia makubaliano ya kibiashara na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, huku lengo ikiwa ni Uendeshaiji wa Kampeni ya kutangaza huduma mbalimbali za Posta zinazotolewa kwa wananchi.

Makubaliano hayo yamefanyika tarehe 09 Februari, 2024 katika Ofisi za ZBC, visiwani Zanzibar huku utiaji wa saini ukifanywa na Postamasta Mkuu, Bw. Maharage Ally Chande pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, Bw. Ramadhan Bukini.

Aidha, hafla hiyo ilihudhuriwa na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Maafisa kutoka Shirika la Posta Tanzania pamoja na ZBC.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano
Shirika la Posta Tanzania,

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA