Habari
POSTA KITAA

Shirika la Posta Mkoa wa Dar es Salaam limekuja na Kampeni Maalumu ya Matangazo ijulikanayo kwa jina la "Posta Kitaa"
Kampeni hii inalenga Kuwajulisha Wateja na Wadau mbalimbali kuhusu huduma Mpya za Posta na zile za zamani zilizoboreshwa na kuwa za kidijitali ili kuhakikisha zinafika Mtaani Kwako.
Katika awamu hii ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutangaza huduma ya Masanduku ya Barua kwa kupita katika mitaa mbalimbali (Road Show) katika Jiji la DSM na Wilaya zake zote.
Ndiyo maana tunasema
"Posta Kitaa twende kidijitali hadi Mtaani Kwako"