JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA YASHIRIKI  KONGAMANO


Shirika la Posta Tanzania limeshiriki Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma la mwaka 2026, linalofanyika kuanzia leo Julai 29 hadi Julai 31, 2026. 

Katika Kongamano hilo  Shirika limekuwa moja ya wadhamini na limetunukiwa Tuzo ya Udhamini kwa kutambua ushiriki wake katika kufanikisha kongamano hilo.

Tuzo hiyo imepokelewa na Meneja wa Posta Mkoa wa Arusha, Bw. Athumani Msilikale, kwa niaba ya Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania.

Kupitia kongamano hilo, Shirika la Posta linatoa huduma mbalimbali pamoja na elimu kwa umma kuhusu fursa na huduma zinazotolewa na Shirika, zikiwemo huduma za Posta, Swifpack, EMS, pamoja na usafirishaji wa mizigo mikubwa kupitia PostCargo, huduma zinazorahisisha shughuli za wananchi na taasisi.

Ushiriki wa Shirika la Posta katika kongamano hilo unalenga kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi, kuongeza uelewa kuhusu huduma zake, pamoja na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali katika sekta ya ununuzi wa umma na maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Wananchi na wadau wote wanakaribishwa kutembelea banda la Shirika la Posta Tanzania ili kupata huduma, ushauri na kufahamu fursa mbalimbali zinazotolewa na Shirika katika kipindi chote cha kongamano.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA