JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA YAFANYA MAFUNZO YA MFUMO WA PSTM


Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Arubee Ngaruka amefungua rasmi mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa usafirishaji sampuli Posta Sample Transportation Management (PSTM).

Mafunzo hayo maalum kwa Waratibu wa Huduma za Maabara wa Mikoa (RLT) kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania bara, yamefanyika kuanzia tarehe 27-29 Aprili, 2026 mkoani Morogoro yakilenga kuwajengea uwezo washiriki katika matumizi sahihi ya mfumo wa PSTM ili kuboresha usimamizi wa usafirishaji sampuli za maabara, kuongeza uwazi, uwajibikaji pamoja na ufanisi katika utoaji wa huduma.

Bw. Arubee ambaye alimwakilisha Postamasta Mkuu , Bw. Macrice Mbodo katika ufunguzi huo alisisitiza kuwa mfumo wa PSTM ni nyenzo muhimu katika mageuzi ya kidijitali yanayolenga kuimarisha ufuatiliaji wa huduma, usimamizi wa taarifa pamoja na kurahisisha mawasiliano kati ya wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa usafirishaji sampuli za kibaolojia kutoka vituo vya afya hadi maabara za uchunguzi.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali muhimu, akiwemo Mkuu wa Huduma za Maabara nchini kutoka Wizara ya Afya, mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, pamoja
na wadau wa maendeleo (Implementing Partners).

Aidha, mafunzo hayo yanajumuisha vipengele vya nadharia na vitendo, ambapo washiriki wanapata fursa ya kutumia mfumo huo moja kwa moja, pamoja na kushiriki katika majadiliano ya changamoto na mbinu bora za kuboresha utekelezaji wake katika mazingira halisi ya kazi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA