JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA YAPONGEZWA


Kamati ya Bunge la Uganda inayoshughulikia masuala ya Posta wamelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa ubunifu wao kutoa huduma za Posta kidijitali huku likihakikisha linakidhi mahitaji ya wateja.

Hayo yamejiri leo tarehe 14 Februari 2025, wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za utendaji zinazofanywa na Posta Tanzania.

Katika ziara hiyo Mkurungenzi wa Biashara Mtandao na Huduma za Uwakala Bw. Contantine Kasese alipata nafasi ya kutoa wasilisho kuhusu Historia ya Shirika, shughuli za utendaji, huduma zinazotolewa na Shirika, Mageuzi ya kidijitali yanayoendelezwa na Shirika pamoja na Mpango mkakati wa Shirika katika kutoa huduma zake. 

Kwa upande wake, Kiongozi wa msafara huo Mhe. Nakut Faith Mbunge wa Bunge la Uganda, amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa jitihada za kuboresha huduma zake kidijitali ili kukidhi mahitaji ya wananchi yanayobadilika kulingana na na maendeleo ya Teknolojia.

Aidha, Mhe. Nakut Faith (Mb) ambae ni kiongozi wa msafara huo aliongozana na Tayebwa Herbet Mbunge wa Uganda pamoja na Jacqueline Muhimbise Karani Mwandamizi wa Mbunge la Uganda.

Katika hatua nyingine, Wajumbe hao walipata nafasi ya kutembelea Kituo cha Huduma Pamoja kinachotoa huduma mbalimbali za Serikali kilichopo katika Ofisi za Posta Kuu Dar es salaam na kujionea namna Posta inavyotoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wananchi 

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Oparesheni Mha. Clarence Ichwekeleza kwa niaba ya Postamasta Mkuu wakiambatana na Menejimenti ya Shirika hilo. 


Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA