Habari
TIMU YA MAUZO POSTA YAFANYA KAMPENI
Timu ya Mauzo ya Shirika la Posta Tanzania imeendelea kufanya kampeni ya kutembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma 2026 kwa lengo la kutangaza huduma za Shirika.

Kampeni hiyo imewezesha wadau wengi kupata uelewa kuhusu huduma za Posta, Swifpack, EMS na PostCargo pamoja na fursa zinazopatikana kupitia Shirika la Posta Tanzania.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

