Habari
POSTAMASTA MKUU AFANYA KIKAO KAZI WUMU
Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo, amefanya kikao kazi na Waziri pamoja na Menejimenti ya Wazara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi (WUMU), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Wizara hiyo tarehe 13 Novemba 2024.
Kikao hicho kimefanyika kufuatia uteuzi wake uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 2 Septemba, 2024.
Lengo kuu likiwa kujitambulisha na kuomba baraka za Wizara hiyo katika mikakati anayotarajia kutekeleza ili kuwahudumia wananchi wa Tanzania ikiwemo visiwani humo ikizingatiwa ni Shirika la Muungano.
Kwa upande wake Dkt. Khalid alishukuru kwa juhudi zinazofanywa na Shirika za kuhakikisha huduma bora na kuwahudumia wananchi wa Zanzibar kwa ufanisi hasa wakati huu wa maendeleo ya kidijitali.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Bi. Habiba Hassan Omar. alisisitiza kuwa huduma ziende sambamba na zitumie vyema miundombinu iliyopo tayari kama vile anwani za makazi. Katibu Mkuu alieleza utayari wa Wizara kushirikiana na Shirika la Posta ili liweze kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania