Habari
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA POSTA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Shirika la Posta Tanzania wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), iliyofanyika Julai 13, 2026, katika Viwanja vya Sabasaba.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mwinyi alipokelewa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Ferdinand Kabyemela Kwa niaba ya Postamasta Mkuu.

Akiwa katika banda la Posta, Mhe. Dkt. Mwinyi alipewa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika, ikiwemo usafirishaji, ubadilishaji wa Fedha, huduma za fedha na uwakala, huduma pamoja na huduma nyingine zinazolenga kuongeza ufanisi, kurahisisha upatikanaji wa huduma na kukidhi mahitaji ya wateja.

Baada ya kupokea maelezo hayo, Mhe. Dkt. Mwinyi amepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Posta Tanzania katika kuboresha huduma zake, akieleza kuwa juhudi hizo zina mchango mkubwa katika kurahisisha biashara, kuongeza upatikanaji wa huduma na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Akizungumza na Rais. Mhe. Mwinyi, Bw. Kabyemela, amesema kuwa, Posta inaendelea kutekeleza maboresho ya huduma na kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ili kuimarisha na kuchangia ukuaji wa biashara na uchumi wa Taifa.

Imeandaliwa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

