JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

PSSF YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI TPC


Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma  (PSSSF), umeendesha mafunzo ya maandalizi ya kustaafu kwa watumishi wa Shirika la Posta Tanzania, Makao Makuu ya Posta, Jijini Dar es salaam, yenye lengo la kuwajenga watumishi baada ya kustaafu.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Utumishi wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Amwesiga Kamihanda, amesema, mafunzo ya maandalizi ya kustaafu kwa watumishi wa Umma yanalenga kuwajengea uelewa mpana kuhusu maisha ya baada ya utumishi na namna bora ya kusimamia mafao yao kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yameendeshwa na wawezeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSF), Bi. Fortunata Pinda na Bw. Iddy Kibire, ambapo waliwapatia watumishi elimu kuhusu umuhimu wa maandalizi ya mapema kabla ya kustaafu, ikiwemo upangaji mzuri wa fedha, uwekezaji sahihi na namna ya kuendeleza ustawi wa maisha baada ya utumishi wa umma. 

Wawezeshaji hao wamefafanua kuwa maandalizi ya kustaafu ni jambo muhimu kwa kila mtumishi, hususani wale wanaokaribia kustaafu, kwani husaidia kupunguza changamoto za kiuchumi na kijamii zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu. 

Aidha, waliwahimiza watumishi kutumia vizuri elimu waliyoipata ili kupanga maisha yao kwa uangalifu, kuhakikisha mafao yao yanatumika kwa tija na kuleta maendeleo binafsi na ya familia.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA