JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TANZANIA YANG’ARA UCHAGUZI WA PAPU


Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania imechaguliwa kuongoza Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika kwenye uchaguzi uliofanyika wakati wa Baraza la 42 la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) vilivyofanyika tarehe 11-12 Juni, 2024 jijini Arusha.

Katika uchaguzi huo Bw. Maharage Chande, ambaye ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania amepata nafasi hiyo ya kuiwakilisha Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa pili wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na wajumbe wote wa Baraza la Utawala waliokuwepo.

Tanzania imeungwa mkono na nchi zote 23 za Baraza hilo zilizokuwepo wakati wa uchaguzi huo. Kupitia nafasi hiyo Tanzania itakuwa na nafasi ya kuongoza vikao hivyo vya juu katika Uongozi wa PAPU. Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Algeria na Makamu wa Kwanza ni Burkinafaso.

Shirika la Posta tunampongeza Bwana Maharage na kumtakia majukumu mema katika nafasi hiyo mpya.

Tanzania imeendelea kung’ara kimataifa kwa kushika nafasi mbalimbali katika nyanja za posta Kimataifa ikiwemo Umoja wa Posta Duniani ambapo Tanzania ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati namba 2 ya Baraza la Uendeshaji, Umoja wa Watoa Huduma za Posta Kusini mwa Afrika (SAPOA) Tanzania ndiye Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo na sasa imepata nafasi katika Umoja wa Posta Afrika.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA