JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

BODI YAPONGEZA MAFANIKIO


Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania imewapongeza viongozi na wafanyakazi wa Shirika kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji yaliyopatikana mwaka wa fedha 2024/2025.

Pongezi hizo zimetolewa na Bw. Toyi Ruvumbagu, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika  alipomwakilisha Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Meja Jenerali (Mst), Gaudence Milanzi alipofungua kikao cha Postamasta Mkuu na wafanyakazi cha robo ya tatu ya mwaka 2025/2026.

Bw. Toyi amesema Serikali imeridhishwa na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Shirika katika utoaji wa huduma na utendaji kibiashara na kuelekeza maandalizi ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tisa wa Kibiashara wa Shirika yakamilike kabla ya Julai 1, 2026.

Aidha, Bodi imetoa maelekezo mawili muhimu kwa viongozi na wafanyakazi wote ikiwemo kuhakikisha wanatimiza malengo ya uzalishaji wa mapato na faida kabla ya kufungwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na kuandaa hesabu za Shirika kwa kuzingatia miongozo yote ya kifedha na kushughulikia hoja zote za ukaguzi kabla ya kuwasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Imeandaliwa na:
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA