JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC NA AZAMPESA NYANDA ZA JUU KUSINI


Shirika la Posta Tanzania wakishirikiana na AzamPesa wamezindua huduma ya AzamPesa kwa ukanda wa nyanda za juu kusini inayohusisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa tarehe 04 Agosti, 2024 katika Banda la Posta lililopo Katika Viwanja vya Maonesho ya nanenane jijini Mbeya.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanywa na Mhe. Benno Malisa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya huku akisisitiza weledi na ubunifu kwa Shirika la Posta Tanzania na AzamPesa katika kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa wananchi hususani wa Ukanda wa nyanda za juu Kusini.

Aidha, Shirika la Posta pamoja na AzamPesa wameahidi kutoa suluhisho la malipo ya kielektroniki kwa kasi na nafuu hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolojia ili kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi nchi nzima.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Taasisi hizi ikiwemo Meneja Fedha na Huduma za uwakala Posta Ahmad Rashid, Meneja Kanda AzamPesa Victor Kihwili, Meneja wa Posta Nyanda za Juu Kusini Michael Mwanachuo, Meneja Kanda Azam Tv Jonas MMbaga, Meneja Azampesa Mbeya Lydia Shirima, Meneja Mkoa wa Njombe Godwin Davis.

Huduma hii ya AzamPesa ni huduma inayowezesha Wananchi kutuma na kupokea fedha pasipo makato yoyote  huku Shirika la Posta likiwa Wakala Mkuu (Aggregator) atakayetoa huduma hii ya AzamPesa katika ofisi zake zaidi ya 300 nchini Tanzania.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA