JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC NA BAHATI NASIBU YA TAIFA


Tunafuraha kutangaza ushirikiano rasmi kati ya Shirika la Posta Tanzania na Bahati nasibu ya taifa ili kukuletea njia mpya na rahisi ya kushiriki.

Kupitia zaidi ya ofisi 207 za Posta nchi nzima, utaweza kununua tiketi, kucheza na kufurahia Bahati Nasibu ya Taifa kwa urahisi katika ofisi ya Posta kilicho karibu nawe.

Ushirikiano huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji na burudani ya michezo ya bahati nasibu kwa Watanzania wote.

Sio tu kuhusu kushinda zawadi, pia ni kuhusu msisimko, burudani, na urahisi wa kucheza wakati wowote, mahali popote!


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA