JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC YANUFAIKA NA UFADHILI WA MAFUNZO


Serikali ya China imetoa ufadhili wa mafunzo ya Uendeshaji katika utoaji wa huduma za Posta kwa Watumishi wanne wa Shirika la Posta Tanzania lengo likiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Posta katika nchi zinazoendelea hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolojia duniani.

Hayo yamebainika katika ziara ya kikazi ya watendaji wa Shirika la Posta Tanzania ambao walikuwa nchini humo kuanzia tarehe 05-13 Juni, 2024 ambapo wamepatiwa mafunzo hayo ili kuleta tija kwa Shirika la Posta Tanzania.

Ziara hiyo iliyofadhiliwa na Serikali ya China kwa nchi zinazoendelea huku ilijumuisha nchi za Tanzania, Cuba, Afghanistan, Mauritius, Armenia na Ethiopia. Shirika la Posta liliwakilishwa na Bw. Ramadhani Mathias Ng'wendankono, Gervas Joel Seth, Waryoba Nyakitita Nyakuwa na Andrea John Liundi.

Katika ziara hiyo watumishi wa Shirika la Posta Tanzania wamejifunza kuhusu Uendeshaji katika masuala ya Posta, Biashara Mtandao, Akili mnemba (Artificial Intelligence) na Matumizi ya teknolojia safi kwenye vyombo vya moto (magari ya umeme na pikiiki za umeme).

Mafunzo mengine waliyoyapata ni pamoja na Umuhimu na matumizi ya Logistics Parks, Umuhimu na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano 5G na 6G, Teknolojia ya kubadilishana taarifa za kibiashara kwa uwazi kupitia mtandao (Blockchain Technology) pamoja na Matumizi ya Pesa Mtandaoni (Cryptocurrency).

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA