JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

POSTA YAPATA TUZO


NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA UCHUKUZI NDUGU SHOMAR O. SHOMAR AFUNGUA MAFUNZO YA TEMESA

Maafisa usafirishaji wa Taasisi za Umma wanatakiwa kusimamia nyezo za kusaidia utendaji kazi Serikalini ili kuimarisha ufanisi na utendaji kazi na utunzaji wa mali za Umma." Hayo yamebainishwa Tarehe 29 Septemba 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasilianona Uchukuzi Zanzibar Bw. Shomar Omar Shomar wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha wadau wanaotumia huduma za Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kilichofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Visiwani humo huku kikao hicho kikiwalenga maafisa Usafirishaji ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaosimamia magari yote ya Serikali katika Taasisi zao.

Katibu Mkuu amewataka maaafisa Usafirishaji hao kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanasimamia vizuri masuala ya usafiri na huduma za ufundi. ‘’Hivi sasa Serikali ipo katika utaratibu wa kuandaa muongozo wa matumizi mazuri ya magari ya Serikali . Hivyo basi kila Katibu Mkuu na Mtendaji Mkuu ana wajibu wa kuhakikisha gari zote zilizo chini ya Taasisi yake anazisimamia vizuri.’’ Amesema Katibu Mkuu ambapo pia amegusia masuala mazima ya nyenzo za utendaji kazi ambazo ni mpango mkuu wa Taifa unaohusiana na masuala ya usafirishaji hasa ufundi na matengenezo ya magari. Shirika la Posta kama mdau mkubwa wa usafirishaji nchini, lilipata nafasi ya kushiriki Mafunzo hayo yaliyofanyika siku mbili na kupokea Tuzo ya Kutambua mchango wao kama Mdau Mkubwa wa ufanyaji kazi na Temesa, Ambapo Tuzo hiyo ilipokelewa na Afisa Usafirishaji wa Posta Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Bakari Abdallah.

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA