JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC YASHIRIKI MBIO ZA FIGO


Shirika la Posta Tanzania laungana na The Healthier Kidney Foundation, Taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kushiriki mbio za FIGO Marathon leo tarehe 22 Septemba, 2024 jijini Dar es Salaam. Malengo ya mbio hizo ikiwa ni kuchangia fedha kwa ajili ya huduma za kuwasaidia watoto wenye matatizo ya Figo  kwa hatua za awali nchini Tanzania.

Mgeni Rasmi katika tukio hilo alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Dkt. Mohammed Mang'una kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama. Dkt. Mang'una amewapongeza wakimbiaji wote kwa ushiriki wao ambao unaboresha afya zao na kuwezesha matibabu ya watoto wenye mahitaji maalum kama hayo.

Kwa upande wake Meneja Posta Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ferdinand Kabyemela amewasisitiza wana Dar es Salaam kujali afya zao na kuendeleza utaratibu wa kufanya mazoezi.

Aidha Bw. Kabyemela pia alizungumzia mageuzi yanayoendelea katika Shirika la Posta na kuwahamasisha Watanzania kuendelea kutumia huduma bora zinazotolewa na Shirika.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA