Habari
TPC YAENDELEZA HUDUMA MSINGI BEI NAFUU

Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania limeeleza kuwa jukumu la kutoa huduma za msingi kwa bei nafuu, inayolingana nchi nzima na inayopatikana kote nchini, lakini pia linapaswa kujiendesha kibiashara ili kuleta tija kwa Shirika la hilo kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Bwana Jasson C. Kalile, Afisa Mwandamizi Mkuu - Idara ya Mawasiliano (Posta), Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, wakati akijibu swali wakati wa Kongamano la Viongozi la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) tarehe 23 Juni, 2025, katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya PAPU jijini Arusha.
Aidha Bw. Kalile aliongeza kuwa vilevile Bei za huduma za Posta hudhibitiwa na mara nyingi huwa chini ya gharama halisi, hivyo huhitaji fidia ili liwe na uwezo wa kishindana kibiashara.
Ikumbukwe kuwa Kwa sasa, Tanzania inafanya tafiti mbili, ambapo moja ikiongozwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kuhusu utoaji wa huduma za msingi, na nyingine inafanywa na Mfuko WA Mawasiliano Kwa wrote (UCSAF ) kuhusu namna ya kusaidia kutekeleza USO. Matokeo tafiti hizo yatasaidia Tanzania na nchi nyingine za Afrika kukokotoa gharama halisi za huduma za msingi za Posta.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania