JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TPC YASHIRIKI MAONESHO TAIC2024


Shirika la Posta Tanzania limeungana na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, pamoja na Taasisi Binafsi kushiriki kwenye Maonesho ya Kongamano la 8 la TEHAMA Tanzania (TAIC2024)  leo tarehe 15 Oktoba, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo alikuwa Mhe. Jerry William Silaa ( Mb), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye aliambatana na Mhe. Marryprisca Mahundi(Mb) Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari   pamoja na Bw. Mohammed Khamis Abdulla Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Wakati wa hafla hiyo, Mhe. Silaa alipata  nafasi ya kutembelea banda la Shirika la Posta Tanzania na kuelezewa safari ya mageuzi ya kidijitali kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA Bw. Michael Njau.

Mhe. Silaa amelipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa Mageuzi yanayoendelea kufanyika ndani ya Shirika ili kuhakikisha utoaji huduma bora kwa wananchi.

Maonesho hayo yanafanyika kwa Siku tano kuanzia tarehe 13 hadi 17 Oktoba 2024. 

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

Rudi Juu

© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA