JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

TUZO YA UDHAMINI WA MAONESHO SABASABA


Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo akipokea tuzo ya udhamini wa Maonesho ya Sabasaba kutoka kwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi tarehe 7 Julai, 2025 katika Ufunguzi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.  

Tuzo hiyo ni kutambua mchango wa Shirika la Posta Tanzania katika kufanikisha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza uchumi wa kidijitali na huduma bora kwa jamii.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA