JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

ZIARA YA MHE. ANGELLAH KAIRUKI POSTA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki akiambatana na Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe. Switbert Mkama wakiwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa ziara ya kikazi leo tarehe 27 Novemba, jijini Dar es Salaam.

                      

Aidha, Ziara hiyo inalenga kufahamu utekelezaji wa majukumu ya Shirika, mafanikio, changamoto pamoja na mikakati ya kuimarisha huduma za Posta nchini. 

                       

Mhe. Kairuki alipokelewa na Postamasta Mkuu, Bw. Macrice Mbodo, pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA