JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

WAZIRI SILAA ATUMIA BODABODA YA POSTA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa akiwa katika Pikipiki ya Shirika la Posta Tanzania ameongoza msafara wa pikipiki na bajaji katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Anwani za Makazi inayofanyika viwanjani hapo jijini Dodoma.

Shirika la Posta Tanzania linashiriki Maonesho ya siku tatu ya Wiki ya Anwani za Makazi yaliyoanza Februari 6, 2025 hadi Februari 8, 2025 katika Viwanja hivyo vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA